UJIO WA ASKOFU ANTHONY FALLAH BORWAH KUTOKA LIBERIA
Mhashamu Askofu Anthony Fallah Borwah akiwa na mwenyeji wake Mhashamu Askofu T Ngalalekumtwa pamoja na Mama Mkuu CST na wanajubilei baada ya misa ya tarehe 08. Des.2018.
Makaribisho ya Askofu Anthony kadiri ya utamaduni wa wanairinga.Amekaa kwenye kigoda mbele yake wazee wawili wakiwa tayari kumvalisha migolole ya kihehe.
Hiyo ni hatua ya kwanza kuvaa nguo hiyo kichwani kama anavyoonekana.
Hatua ya pili anavalishwa lubega ndiyo mtindo wa wazee wa kihehe.Asante Mzee Malangalila kwa kuuenzi utamaduni wa Wahehe.
Karibu sana nyumbani kwa Wateresina Baba Anthony. Ni maandamano ya kuanza misa ya shukrani kwa Mungu kwa ujio wa Mzee wetu.
Shamra shamra baada ya misa ya shukrani kwa pamoja kifamilia.
Katika kituo cha watoto Yatima Tosamaganga.
Fahari ya Taifa ni mbuga za wanyama. Hapa tukiwa na mgeni wetu baada ya kutoka ndani ya hifadhi ya Ruaha National Park.Tunamwombea afya njema na safari njema ya kurudi Liberia.